27.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

TANZANIA YATUNUKIWA TUZO YA MAPAMBANO YA MALARIA

 

Na Veronica Romwald, Dar es Salaam

Tanzania imetunukiwa tuzo ya mapambano dhidi ya ugonjwa wa malaria na Shirika la Afya Duniani (WHO) kwa kutambua juhudi zake za kupambana na ugonjwa huo.

Tuzo hiyo imekabidhiwa leo Jumatatu Februari 26, kwa Mganga Mkuu wa Serikali, Profesa Mohamed Kambi na Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkaazi wa WHO, Ritha Njau, jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari, Profesa Kambi amesema kutokana na juhudi mbalimbali zilizofanywa na serikali kiwango cha maambukizi ya malaria nchini kimepungua kutoka kesi milioni 18 mwaka 2008 hadi kufikia milioni 5.5.

“Idadi ya vifo vya watoto chini ya miaka mitano imepungua kutoka vifo 102 kwa kila vizazi hai 1,000 hadi kufikia vifo 67 kwa kila vizazi hai 1,000.

“Ugonjwa wa malaria ni miongoni mwa magonjwa yaliyochangia idadi kubwa ya vifo hivyo lakini kwa kuwa tumeudhibiti imesaidia kupungua vifo hivyo,” amesema Profesa Kambi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles