19.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, October 4, 2022

Serikali yasema michango ya ajali MV Nyerere iko sehemu salama

Mwandishi Wetu, UkereweSerikali imesema fedha zote zilizochangwa kwa ajili ya ajali ya kuzama kwa Kivuko cha MV Nyerere, zimehifadhiwa sehemu salama.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama, amesema hayo leo katika Kijiji cha Bwisya, wilayani Ukerewe akitoa salamu katika mazishi ya halaiki.

Amesema fedha hizo zilizochangwa na Watanzania na wasio Watanzania zinahifadhiwa sehemu salama kwa shughuli husika na tayari imefunguliwa akaunti kwa ajili hiyo.

“Pia tutafungua akaunti ya Tigopesa ili watu waendelee kuchangia na kama nilivyosema awali zitafanya shughuli husika,” amesema Jenista.

Pamoja na mambo mengine, amesema pamoja juhudi zilizofanywa na wananchi na watu mbalimbali serikali imefanya kazi kubwa ikiwamo kutoa mchango mkubwa wa vifaa tiba kwa walionusurika na kuhifadhi waliofariki.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
202,660FollowersFollow
554,000SubscribersSubscribe

Latest Articles