22.2 C
Dar es Salaam
Monday, October 14, 2024

Contact us: [email protected]

Serikali yarudisha kodi kwenye taulo za kike

Asha Bani -Dar es Salaam

Serikali imesema itarudisha kodi ya wanaoagiza taulo za kike endapo hawatashusha bei.

Hatua hiyo imefikiwa kutokana na wauzaji na wasambazaji wa taulo hizo kushindwa kupunguza bei zake itakayomsaidia mwanafunzi kumudu gharama.

Hayo yameeelezwa leo Februari 15, na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu wakati akifungua mkutano wa siku mbili  wa kupinga mimba za utotoni uliyoandaliwa na Taasisi ya Girls Inspire kutoka nchini Canada kwa kushirikiana na Australia, ambao umewakutanisha wadau mbalimbali wa elimu.

Amesema Amesema tayari amemwandikia barua Waziri wa Viwanda na Biashara pamoja na Waziri wa Fedha na Mipango, kuanza kushirikiana kusimamia suala hilo ikiwa ni pamoja na  kupunguza gharama na kuongeza idadi ya taulo hizo badala kuweka sita au nne waweke nane au 10.

“Tuliwapunguzia kodi waingizaji na watengenezaji wa taulo hizo kuhakikisha wanashusha gharama,  bei haijapungua kabisa hivyo inabidi tuirudishe maana haijaleta tija kwa watanzania hasa watoto waliopo vijijini ambao hawana uwezo wa kununua taulo hizo kwa kiasi cha Sh 2,000 jambo ambalo hatutalivumilia ,” amesema Waziri Ummy.

Amesema takwimu zilizopatikana baada ya utafiti uliofanywa  na Serikali mwaka 2015/16 zinaonesha kati ya watoto wa kike 100 kati yao 27 wamepata mimba  wakiwa na umri chini ya miaka 18 ambapo  licha ya watoto hao kupata mimba lakini pia wamesababishiwa matatizo mbalimbali ya kiafya.

Amesema madhara ya ndoa na mimba za utotoni nchini ni makubwa kwani licha ya mtoto wa kike kupata matatizo ya kiafya pia husababisha kundi hilo kukosa elimu na hatimaye kuwa maskini kwa kushindwa kutimiza ndoto walizojiwekea. 

Aidha Waziri Ummy ameongeza kuwa serikali imejitahidi kuchukua hatua mbalimbali kudhibiti hayo yasiendelee ikiwa ni pamoja na kuanzisha sera ya elimu bure iliyoongeza fursa za watoto wa kike na kiume kupata elimu za msingi na sekondari.

Naye Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia William Ole nasha amesema ndoa na mimba za utotoni zinamfanya mtoto wa kike ashindwe kusonga mbele hivyo serikali itaendelea kuchukua hatua madhubuti kuhakikisha watoto wa kike wanabaki shuleni na kutimiza ndoto zao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles