28.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Kubenea atoa msaada wa madawati shule za Ubungo

Asha Bani -Dar es Salaam

Mbunge wa Ubungo Saed Kubenea amekabidhi jumla ya madawati 290 yenye thamani ya zaidi ya Sh milioni 28 yatakayokwenda kugawanywa katika shule mbalimbali zilizopo jimboni mwake.

Akikabidhi madawati hayo leo Februari 15, katika shule ya sekondari Mashujaa amesema amefanya hivyo kutokana na kuona umuhimu wa wanafunzi hao kusoma katika mazingira yaliyo bora zaidi.

Amezitaja shule zitakazopatiwa mgao wa madawati hayo kuwa ni shule za Makoka, Makuburi, na Mabibo zitakazopata madawati 30 na viti 30 na Mashujaa itakayopata madawati 50 na viti 50.

Naye Mkuu wa shule ya sekondari ya Mashujaa Edda Kondo,amemuelezea mbunge huyo changamoto iliyopo shuleni hapo kuwa ni pamoja uhitaji wa ukarabati wa vyumba 17 na kutokuwa na maabara, vifaa vya sayansi na vitabu.

“Kwa kua shule ni mpya haina vitabu vya masomo yote ya kufundishia pamoja na vifaa kama vile chaki ,vifaa vya kutengeneza zana za kufundishia, kalamu na vinginevyo.

“Tukumbuke kuwa Tanzania yetu ya viwanda na teknolojia hivyo tunahitaji vitendea kazi kama vile mashine za kutoa chapa na kuchapia  kwa ajili ya matumizi ya ofisi kama kuchapisha mitihani na mazoezi ili kupandisha taaluma ya wanafunzi,”amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles