24.8 C
Dar es Salaam
Friday, October 4, 2024

Contact us: [email protected]

Serikali yapiga marufuku utupaji plastiki, taka ngumu

SNa MWANDISHI WETU-NJOMBE

NAIBU Waziri wa  Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mussa Sima, ameziagiza mamlaka zinazohusika na ubebaji wa taka ngumu nchini kuhakikisha wanatenganisha chupa za plastiki na taka nyingine kwa sababu zikichanganywa na taka ngumu na kutupwa  kwenye dampo na hivyo kuharibu mazingira.

Akizungumza akiwa mkoani Njombe wakati akitembelea dampo za uchafu katika Halmashauri ya Miji ya wilaya za Mkoa wa Njombe, Naibu Waziri Sima alisema kuchanganya chupa za plastiki kwenye uzoaji taka na kwenda kuzitupa katika madampo, zina athari kubwa ya kimazingira kwani  haziozi.

“Changamoto nyingine ni hizi chupa za plastiki ni nyingi, zinakusanywa na kuzihifadhi mahali kwa kuwa kuna biashara inafanyika ya hizi chupa za plastiki, sasa tunatoa uchafu nje tunauleta mahali ambapo tunajua tunauteketeza, wapo wengine wanakuja wanautoa ule uchafu kwa kupitia hizo chupa za plastiki,” alisema Sima.

Alisema Serikali kupitia Baraza la Uhifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), itaratibu na  kusimamia utekelezaji  wa agizo hili kwani kuna sheria na kanuni zinazowaongoza kutekeleza majukumu yao.

Alisema ziara yake mkoani Njombe ililenga kuona halmashauri zinazosimamia usafi wa mazingira, zinateketeza kwa kiasi gani taka ngumu ili zisilete athari ya mazingira.

“Nataka nione ni kwa kiasi gani wanateketeza zile taka hatarishi na pia ni kwa namna gani haya madampo yalivyo mbali na makazi ya wananchi pamoja na maji taka yanayotoka kwenye makazi ya wananchi yanaenda wapi.

“… hii yote tunataka kuipunguzia mzigo Serikali kwani yapo magonjwa yanayotokana na uchafu na kuwakumba wananchi ambao watahitaji kutibiwa na Serikali, hivyo sasa tunapaswa kuipunguzia mzigo,” alisema Sima.

Kwa upande wake, Mratibu wa Baraza la Uhifadhi wa Mazingira (NEMC), Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Godlove Mwamsoje, alitoa wito kwa Watanzania kuhakikisha wanasimamia vyanzo vya maji na kuvitunza.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles