24.1 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

RC kuendesha operesheni ya kudhibiti maadili

RNa KHAMIS SHARIF-ZANZIBAR

MKUU wa Mkoa wa Mjini Magharibi, Ayoub Mohammed Mahmoud, amesema Serikali ya mkoa itaendelea kufanya operesheni za mara kwa mara ili kudhibiti vitendo vinavyoashiria mmomonyoko wa maadili kwa vijana.

Akizungumza mwishoni mwa wiki wakati akifungua kikao cha pamoja cha kujadili namna ya kuendeleza mapambano dhidi ya maradhi hayo kwa kamati za kupambana na Ukimwi za Manispaa ya Mji wa Zanzibar na Makamishna wa Tume ya Ukimwi Zanzibar (ZAC), ambapo alisema ili kufikia lengo la kuipata 90 tatu, ni lazima kamati hizo zianze kuangalia upya viashiria vinavyopelekea maradhi hayo.

Alisema kikawaida miji mikuu ulimwenguni inakuwa na shughuli nyingi zikiwemo zinazochochea mmomonyoko wa maadili na vitendo viovu, hivyo operesheni hizo zinalenga kupunguza madhara ya matendo hayo.

Alisema kutokana na hali hiyo, alibaini kuwepo kwa nyumba za kulala wageni ‘Guest House’ na za binafsi zinazoendesha au kujihusisha na biashara ya ngono, jambo ambalo ni kichocheo kikubwa cha kusambaa kwa maambukizi ya maradhi mbalimbali ikiwemo Ukimwi.

“Kama Serikali, tumebaini kasoro kubwa ya utumiaji  mbaya wa nyumba za kulala wageni, zimekuwa zikitumika vibaya na nyingine hazipo kwa mujibu wa sheria kwani hazijasajiliwa,” alisema. 

Pamoja na hali hiyo, mkuu huyo wa mkoa alikemea tabia ya baadhi ya watendaji wa Serikali na vyombo vya ulinzi na usalama kushirikiana na watu wanaojihusisha na vitendo hivyo, jambo ambalo linapunguza ufanisi.

Ayoub alipongeza juhudi zinazochukuliwa na Tume ya Ukimwi Zanzibar kwa kutoa elimu na usaidizi kwa watu wanaoishi na virusi vya Ukimwi.

Aliwashauri wajumbe wa Tume hiyo wanaotokana na taasisi za dini, kuanzisha utaratibu wa kukutana na viongozi wenzao na kupanga mikakati ya kueneza elimu ya kupambana na maradhi hayo ili kujenga uelewa wa pamoja kwa jamii.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles