SERIKALI YAONYA UPOTOSHAJI MITANDAO YA KIJAMII

1
514

SERIKALI imesema itamchukulia hatua kali za kisheria mtu yeyote aliyesambaza taarifa za upotoshaji kwenye mitandao ya kijamii.

Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari Dar es Salaam jana na Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasilino ya Serikali cha Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Christina Mwangosi, ilisema kumekuwapo na taarifa za uongo zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii zenye kichwa cha habari kinachosema “kanuni na sheria  za Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi zitabadilishwa’.

Taarifa hizo, zimeanza zimeanza kusambazwa  juzi zikidai  kuanzia janana kuendelea  kutakuwa  kuna kanuni  mpya za mawasiliano.

“Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, inapenda kuujulisha umma  kuwa taarifa hii, ni ya uongo na uzushi,haina ukweli wowote na inalenga kuvuruga wananchi…tunaomba waipuuze.

“Wizara inatoa onyo kali kwa mtu yeyote aliyeanzisha na wale wanaoendelea kusambaza taarifa hii,hatua kali zitachukuliwa  kwa watu wanaozusha  mambo kwenye mitandao ya kijamii kwa kuwa Serikali inao mfumo rasmi wa utoaji wa taarifa  kwa kutumia mfumo wa “kielectroniki na hardcopy,’’ ilisema taarifa hiyo.

1 COMMENT

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here