24.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 23, 2024

Contact us: [email protected]

ASILIMIA 33 WANAUME DAR WANA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME

ASILIMIA 33 ya wanaume 672 mkoani Dar es Salaam wamebainika kuwa na upungufu wa nguvu za kiume.

Utafiti uliofanywa na Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) kwa wanaume 672 ambapo kila wanaume watatu mmoja aligundulika kukosa nguvu za kiume ambapo pia idadi kubwa walibainika kuwa na magonjwa ya shinikizo la damu na kisukari.

Daktari Bingwa wa Magonjwa ya moyo, Dk. Pedro Pallangyo alisema utafiti huo ni kati ya tafiti 16 zilizompa ushindi wa tuzo ya watafiti vijana wa Afrika kwa mwaka 2016/17 (Young African Researchers Awards 2017) ambapo alifanya katika kipindi cha mwaka mmoja.

“Hali hii inaashiria kuwa magonjwa ya kisukari na shinikizo la damu yamekuwa yakiongezeka mara kwa mara jambo ambalo linasababisha athari ya nguvu za kiume kuwa kubwa,” alisema Dk. Pallangyo.

Pamoja na mambo mengine alisema changamoto hiyo inaweza kutatuliwa iwapo jamii itakuwa na utaratibu wa kufanya uchunguzi wa afya mara kwa mara ili kugundua tatizo mapema na kupata matibabu.

“Kama mgonjwa akiwahi matibabu mapema kabla mishipa ya damu haijaathirika zaidi anaweza kudhibiti sukari na shinikizo la damu na kurudi katika hali yake ya kawaida,” alisema Dk Pallangyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles