23.4 C
Dar es Salaam
Saturday, April 27, 2024

Contact us: [email protected]

Serikali yaendelea kujipanga kuvutia watalii baada ya corona

Na TUNU NASSOR-DAR ES SALAAM

WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangala, amezindua matumizi ya muhuri wa usalama kwa wasafiri nchini uliotolewa na Baraza la Wasafiri na Watalii Duniani (WTTC).

Akizindua muhuri huo Dar es Salaam jana, Kigwangala alisema ni muhimu katika kujenga imani kwa wasafiri na watalii duniani kote kwa kuwahakikishia wako salama wanapokuja nchini.

Alisema kwamba miongozo ya usalama inafanyiwa kazi ili kuwawezesha kusafiri salama bila kupata maambukizi ya ugonjwa wa Covid-19.

“Tutumie muhuri huu kuwathibitishia wadau na watalii kwamba Tanzania ni salama kwa wageni na kujenga tumaini jipya kwa watalii na kutekeleza sera na miongozo ili kurejesha imani kwa kuimarisha tasnia hii,” alisema Kigwangala.

Alisema muhuri huo utatumika kama fursa ya kutengenea watalii wengi katika kipindi ambacho nchi nyingi bado hazijafungua mipaka ya utalii.

Kigwangala alisema Tanzania sasa imeorodheshwa kati ya vituo vilivyo salama duniani na kuthibitishwa na WTTC.

Aliongeza kuwa Juni mwaka huu walizindua mwongozo wa namna ya kuendesha shughuli za utalii katika kipindi cha janga la Covid-19 na sasa umezaa matunda na kupata muhuri huo.

“Uamuzi wa Rais Dk. John Magufuli kufungua mipaka yetu huku tukichukua tahadhari thabiti juu ya janga la Covid-19 umeifanya Tanzania kuwa salama na kupata muhuri huu leo,” alisema Kigwangala.

Alisema kwa hapa nchini hakuna tena ugonjwa wa Covid-19 ndio maana kumekuwa na mikutano na matamasha ya muziki bila kusikia maambukizi mapya, hivyo wageni watakapoingia watatakiwa kupimwa na kufuata masharti ya kujikinga,” alisema Kigwangala.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Utalii nchini (TTB), Devota Mdachi alisema kampuni za usafiri wa anga na mawakala wa usafiri kutoka sehemu mbalimbali duniani walitembelea nchini kuangalia kama ni salama kwa wasafiri na walijiridhisha kuwa ni salama.

“Bodi ilitembelea nyumba za wageni, hoteli na maeneo ambayo hutembelewa na wageni hao na tumejiridhisha kuwa masharti ya kujikinga na ugonjwa wa Covid-19 yanafuatwa kikamilifu.

“Tanzania sasa ni salama na iko tayari kupokea watalii na kuwahakikishia wanakuwa salama mpaka wanaporudi kwao,” alisema Devota.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa bodi hiyo, Jaji mstaafu Thomas Mihayo alisema sekta hiyo ilishirikiana na sekta binafsi kuhakikisha usalama na masharti ya kujikinga na Covid-19 yanafuatwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles