26.1 C
Dar es Salaam
Friday, December 9, 2022

Contact us: [email protected]

Mtaka azuia Magari ya Halmashuari Simiyu kupelekwa TEMESA

Derick Milton, Simiyu

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Antony ameziagiza halmashuari zote mkoani humo kusitisha kupeleka magari yao ambavyo yanahitaji kufanyiwa matengenezo kwa wakala wa ufundi na umeme (TEMESA) mkoani humo kutokana na gharama za wakala huyo kuwa kubwa.

Mbali na hilo mtaka amesema kuwa mbali na gharama kuwa bwana, bado matengenezo yanayofanywa na TEMESA yamekuwa chini ya kiwango na wakati mwingine magari kuharibika zaidi baada ya kutoka kwao.

Mtaka ametoa maagizo hayo leo kwa wakurugenzi wa halmshauri hizo wakati wa kikao cha wadau wa Afya, ambapo amesema ndani ya miezi mitatu mkoa utapanga wapi magari yawe yanapelekwa kutengenezwa.

” Malalamiko dhidi ya TEMESA yamekuwa mengi, gharama zao ni kubwa mno zaidi ya mara tatu, nne ya mafundi wengine wazuri, lakini wakati mwingine hawana mafundi wa kutosha, wanatumia wa mitaani na magari hayatengenezwi vizuri,” Amesema Mtaka.

“Tunajipa kipindi cha miezi mitatu kutafuta njia nyingine sahihi ya wapi tutakuwa tunatengeneza magari yetu, baada ya hapo hakuna kupeleka gari TEMESA, hatuwezi kuwa tunapeleka magari yetu kwa gharama kubwa na hayatengenezwi ipasavyo,” Amesema Mtaka.

Aidha Mtaka amesema kuwa TEMESA wamekuwa wakilalamikiwa kuweka vipuri chakavu na ambavyo havina ubora, kwenye magari ambayo wanapelekewa na halmashuari kwa ajili ya kutengenezwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
205,734FollowersFollow
558,000SubscribersSubscribe

Latest Articles