27.1 C
Dar es Salaam
Wednesday, October 4, 2023

Contact us: [email protected]

Serikali, UNDP kugawa hati za kimila

Na Amina Omari, Korogwe

SHIRIKA la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) kwa kushirikiana na Serikali  linatarajia  kugawa hati za ardhi za kimila 1000  maeneo yaliyo karibu na vyanzo vya maji  kwa mikoa ya Tanga na Morogoro.

Hati hizo ambazo zitatolewa maeneo ya vyanzo vya maji katika mabonde ya Ruvu na Pangani ili kuhakikisha wanalinda uharibifu wa mazingira katika vyanzo hivyo.

Akizungumza wakati wa  uzinduzi wa ugawaji wa hatimiliki ya ardhi za kimila katika Kijiji cha Magunga Cheke wilayani Korogwe, mwakilishi Mkazi wa UNDP, Christine Musisi alisema zitaweza kusaidia kumaliza changamoto ya uharibifu wa vyanzo vya maji unaofanywa kutokana na shughuli za kibinadamu.

Alisema shirika hilo limewezesha mpango huo kwa kuandaa matumizi bora ya ardhi, ikiwamo upimaji wa maeneo  katika vijiji 20 mkoani Tanga.

“Dunia inashuhudia uharibifu mkubwa wa vyanzo vya maji kutoka na shughuli za kibinadamu, uwapo wa mpango huo utasaidia kudhibiti uharibifu kwa kiwango kikubwa,”alisema.

Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tanga,ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Muheza, Mwanasha Tumbo alisema uharibifu wa mazingira unapelekea uhaba wa maji.

Alisema ugawaji wa hati hizo utasaidia matumizi bora ya ardhi ikiwemo uepukaji wa migogoro ya ardhi uliopo hasa katika maeneo ya vijijini pamoja utunzaji wa vyanzo vya maji.

“Kuliwepo na uharibifu mkubwa wa vyanzo vya maji  Mto Zigi ambao ulisababisha uhaba wa maji, baada ya utunzaji wa mazingira hali imebadilika,”alisema.

Mwakilishi wa Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Rosemary Rwebugisa alisema uharibifu katika vyanzo vya maji, umekuwa changamoto kubwa hapa nchini.

“Shughuli za kibinadamu katika vyanzo vyamaji zimekuwa zikichangia uchafuzi wa maji na  kupunguza ubora wake,”alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,770FollowersFollow
575,000SubscribersSubscribe

Latest Articles