23.8 C
Dar es Salaam
Friday, September 22, 2023

Contact us: [email protected]

RC afanya ziara ya kushtukiza hospitali

Na BEATRICE MOSSES-MANYARA

MKUU wa Mkoa wa Manyara, Alexander Mnyeti amefanya ziara ya kushtukiza Hospitali ya Mji wa Mbulu ili kubaini namna wagonjwa wanavyohudumiwa.

Mnyeti alifika hospitali hapo mara mbili saa 9 alasiri  na saa 3 usiku bila uongozi wa hospitali wala wagonjwa kutambua kama amewatembelea.

Awali alifika alasiri na gari lake bila bendera na kutembelea wodi walikolazwa wagonjwa na kuzungumza nao ili kutambua namna wanavyopatiwa huduma.

Alizungumza pia na wauguzi waliokuwepo ambapo aliwahoji namna wanavyotoa huduma ikiwemo lugha nzuri kwa wagonjwa ili wapate faraja wakati wakitibiwa.

Akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Gedamar, Nyeti  alisema lengo lake lilikuwa ni kujua namna wagonjwa wanavyohudumiwa kuliko kusubiri kuambiwa.

“Nimefika hospitali na kukuta baadhi ya upungufu lazima ufanyiwe kazi, wauguzi usiku inakuwa shida kuhudumia wagonjwa, nimeshuhudia mwenyewe,” alisema Mnyeti.

Alisema dirisha la wazee inaonyesha wameweka karatasi muda siyo mrefu, baada ya kupata taarifa ya yeye kuanza ziara wilayani Mbulu.

“Mganga mkuu nakuagiza nakuagiza kasimamie hospitali yako vizuri, kuna mambo hayajakaa sawa karatasi la dirisha la wazee limewekwa cjui juzi sisi tumekuta karatasi mpya”,alisema Mnyeti.

Mkuu wa Wilaya ya Mbulu, Chelestino Mofuga alisema wanayapokea upungufu huo na kuhakikisha watayafanyia kazi.

“Tunakuahidi  upungufu  mdogo tumeuchukua na tunakuhakikishia tunaufanyia kazi  haraka,” alisema Mofuga.

Mmoja wa  wagonjwa, John Tsere alisema kitendo cha mkuu wa mkoa kutembelea kwa kushtukiza hospitalini hapo kitaongeza uajibikaji kwa wauguzi na madaktari.

“Amefika bila polisi wala viongozi wa wilaya, amevaa nguo za kawaida yaani huwezi kubaini kama ni mkuu wa mkoa wakati mwingine ni vizuri kufanya hivi ili uone mwenyewe kuliko kusomewa taarifa,” alisema Tsere.

Mnyeti yupo kwenye ziara ya siku nne wilayani Mbulu  kukagua miradi ya maendeleo, kuzungumza na wananchi na kusikiliza changamoto zinazowakabilia.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,690FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles