26 C
Dar es Salaam
Monday, March 4, 2024

Contact us: [email protected]

Serikali: Kuna udhaifu kwenye kupambana na nzige

Na Upendo Mosha, Moshi

Serikali imesema hairidhishi na utendaji wa shirika la kukabiliana na nzige wa jangwani la Afrika Mashariki lenye makao yake makuu nchini Ethiopia, kutokana na udhaifu katika kupambana na nzige hao ambao wameendelea kuathiri nchi wanachama wanaohudumiwa na shirika hilo.

Aidha serikali imeelezea kusikitishwa kwake na hatua ya Mtendaji Mkuu wa Shirika hilo, Dk. Nzoka pamoja na kupewa taarifa kwamba Waziri wa Kilimo wa Tanzania,Prof Adolf Mkenda anamtafuta lakini bado hajaoneshwa kujali taarifa hiyo.

Waziri Mkenda amesema kutokana na udhaifu huo, serikali kupitia Wizara ya Mambo ya Nje imewasiliana na Balozi wa Tanania nchini Ethiopia na kumuelekeza amtafute Mkuu wa Shirika hilo kujua tatizo liko wapi.

“Haiingii akilini kwamba tunaomba msaada katika shirika la nzige wekundu wakati, shirika la kupambana na nzige wa jangwani halitekelezi wajibu wake….tumechukua Helkopta na ndege ya kukabiliana na nzige wekundu, huku hii ya kwetu imepaki hapa uwanja mdogo Moshi na haina rubani,” amesema.

Amesema ndege ya kukabiliana na nzige wa jagwani ipo katika uwanja wa Moshi huku rubani wake akipelekwa Kenya jambo ambalo linatia shaka kuhusu utendaji wa shirika hilo hususan kipindi hiki ambacho nchi wanachama limevamiwa na nzige wa jangwani.

“Kama utendaji wa shirika hili uko hivi, haishangazi kuona nzige hawa wanaendelea kuathiri nchi wanachama na hakuna jitihada za makusudi kuwakabili…ikumbukwe Tanzania ni moja ya nchi mbili ambazo zinalipa vizuri ada zake za uanachama wa shirika hilo,”amesema.

Aidha Waziri Mkenda amesema mapambano dhidi ya wadudu hao yanaendelea vyema kwa kushirikiana serikali ya Kenya kutokana na ukweli kwamba nzige hao wanauwezo wa kutembea Km 80 kwa siku hivyo ni rahisi kutoka eneo moja hadi jingine.

Aidha alisema serikali imejipanga kikamilifu kuhakikisha nzige hao wanaangamizwa na tayari ndege ya shirika la kupambana na nzige wekundu kutokea nchini Zambia liko Wilaya ya Longido kupambana na nzige hao.

Alisema Kundi jipya la nzige nzige limeingia nchini kutokea Kenya na kwamba lipo Longido na tayari ndege kutoka shirika la kupambana na nzige wekundu lipo tayari kupambana na nao.

Aidha alisema wamepata taarifa kuna kundi jingine limetokea Machakos na kwamba huenda likaingilia upande wa Kajiado na kunaweza kuja Tanzania lakini ambapo tayari wizara imekwisha fanya tunawasiliana na Kenya ili kuweza kuwawahi na kuwaangamiza.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
584,000SubscribersSubscribe

Latest Articles