25.2 C
Dar es Salaam
Monday, April 22, 2024

Contact us: [email protected]

HAI: Takukuru yaagizwa kumsaka aliyekuwa mtendaji wa mtaa

Na Upendo Mosha, Hai

Serikali wilayani Hai, mkoani Kilimanjaro, imeagiza wananchi waliovamia eneo lenye ukubwa wa hekari 22.5, lililopo Mji mdogo wa Bomangombe kuondoka na kuagiza taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa TAKUKURU kwa kushirikiana na jeshi la Polisi kumsaka aliyekuwa mtendaji wa Mtaa huo Sabore Mollel.

Agizo hilo lilitolewa Jana, Mkuu wa wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya, wakati wa ziara yake ya ukaguzi wa eneo hilo lililotegwa kwaajili ya Dampo, lililopo mtaa wa Jiweni,mji mdogo wa Bomang’ombe, wilayani humo, mkoani Kilimanjaro.

Amesema wananchi hao wamekuwa na malalamiko kwa madai kuwa walipewa maeneo hayo na serikali ya Kijiji kuanzia Mwaka 1993 hadi 1993 jambo ambalo lilifanywa kinyume na taratibu za ardhi na kwamba wanapaswa kuondoka .

Amesema mwaka 1984 eneo hilo lilitegwa kuwa sehemu ya mipango miji ya halmashauri ya wilaya hiyo na kwamba 1988 liliingizwa katika mpango kabambe wa Mjini.

Aidha amesema aliyekuwa Mtendaji wa Kijiji hicho, Sabore Moleli, ambaye alifukuzwa kazi Mwaka 2017 kwa vyeti feki, alikuwa akigawa maeneo hayo kinyume na taratibu Jambo ambalo limekuwa likisababisha serikali kuingia katika migogoro na wananchi.

Sabaya pia aliwataka wananchi 15 ambao walipewa maeneo hayo kufika katika Ofisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa kuhojiwa na kueleza namna walivyo yapata.

Mbali na hilo aliiagiza Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri hiyo,yohana Sintoo,kuhakikisha analinda eneo na asiwepo Mwananchi yeyeyote atakaye ingia.

Naye Mkurugenzi wa halmashauri hiyo, Yohana Sintoo, amesema eneo hilo lilitegwa kwaajili ya Dampo na kwamba kwa Sasa lipo chini yao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles