25.1 C
Dar es Salaam
Saturday, May 4, 2024

Contact us: [email protected]

Serikali kuboresha mazingira ya uwekezaji kuzisaidia sekta binafsi kukua

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Serikali imeahidi kuendelea kuboresha na kuimarisha mazingira ya biashara nchini kuzisaidia sekta binafsi kufanya kazi zao kwa ufanisi bila vikwazo, huku ikiwatoa wasiwasi wananchi kuhusu kukamilika kwa miradi ya reli ya kisasa (SGR). 

Hayo yalisemwa Machi 6, 2024  jijini Mwanza na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule wakati akifunga kongamano la biashara na uwekezaji katika sekta ya reli lililofanyika kwa siku mbili, huku akibainisha kwamba kwa kutambua umuhimu wa sekta binafsi serikali imeanza kufanya mabadiliko ya Sheria mbalimbali ambazo zitasaidia sekta hiyo kufanya kazi bila vikwazo. 

Amesema Serikali inatambua umuhimu wa ushiriki wa sekta binafsi katika shughuli za kiuchumi na kazi kubwa ya Serikali ni kutengeneza mazingira wezeshi kwa wao kuwekeza, ambapo Serikali ya awamu ya sita itaendelea kuhakikisha uwepo wa mazingira rafiki ya uwekezaji na kwa wawekezaji wenyewe.  

“Kwa niaba ya Serikali ninapenda kuwahakikishia kwamba Shirika letu la Reli (TRC) litaendelea kusimamia, kuendesha na kuhakikisha kwamba miundombinu ya reli inaimarika na miradi yote inakamilika kwa muda uliopangwa,’’ amesema Senyamule. 

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Masanja Kadogosa amesema kongamano hilo la biashara na uwekezaji katika sekta ya reli limevutia wawekezaji wengi huku baadhi yao wakionyesha nia ya kuwekeza katika usafiri wa treni nchini hususan utoaji wa huduma za kijamii. 

“Kongamano hili limetusaidia kuvutia wawekezaji mbalimbali katika sekta hii ya reli nchini na ukiangalia sekta hii hapa kwetu kuna fursa mbalimbali za kuwekeza ikiwemo ujenzi wa miundombinu ya reli, utoaji wa huduma za uendeshaji na ujenzi wa nyumba na majengo ya kukodisha pembezoni mwa reli zetu,” amesema Kadogosa na kuongeza; 

“Tunawaomba wadau wote wanaovutiwa na kufanya kazi na shirika letu wajitokeze kwa wingi watume maombi na sisi tutayafanyia kazi lengo ni kuhakikisha tunaboresha huduma zetu na kutoa huduma bora kwa wananchi,”.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles