MPENZI wa zamani wa msanii wa Pop, Justin Beiber, Selena Gomez, ametangaza kuuza nyumba yake yenye ukubwa wa mita za mraba 7,700.
Mrembo huyo ameitumia nyumba hiyo kwa mwaka mmoja na nusu, lakini kwa sasa ametangaza kuiuza kwa kitita cha dola milioni 3.7.
Selena alisema sababu za kutangaza kuuza nyumba hiyo ni kwamba mwakani hatokuwa na muda wa kukaa kwenye nyumba hiyo kutokana na ratiba yake kumbana na mizunguko ya kibiashara.
“Ninahisi ninafanya maamuzi sahihi ya kuuza nyumba, kutokana na ratiba yangu kuanzia Januari nitakuwa na mizunguko mingi hivyo nitakosa muda wa kukaa mara kwa mara,” alisema Selena.
Hata hivyo, kuna taarifa zinaenea mitandaoni kwamba mrembo huyo ameanza kuonekana na mpenzi wake wa zamani Beiber, hivyo kuna uwezekano watakuwa wamemaliza tofauti zao.