31.2 C
Dar es Salaam
Saturday, December 2, 2023

Contact us: [email protected]

Nalimi Mayunga: Ndoto yangu kimataifa imetimia

MalimiNA KOKU DAVID

MSANII wa muziki wa kizazi kipya, Nalimi Mayunga ambaye ni mshindi wa shindano la ‘Airtel Trace Music Stars Afrika’, amesema hatawaangusha Watanzania na kwamba ataipeperusha vizuri bendera ya Tanzania nchini Marekani.

Msanii huyo ameondoka jana kuelekea nchini Marekani ambako atafanya kazi na nguli wa muziki wa Rnb duniani, Aliaume Damala ‘Akon’ na atakaa huko  kwa wiki moja.

Akizungumza jijini Dar es Salaam kabla ya kuondoka, Mayunga alisema kuwa ndoto yake ya kufanya kazi ya muziki na wasanii wa kimataifa imetimia na kwamba ataitumia nafasi hiyo vizuri ili aweze kufikia pale anapotaka.

Safari ya Mayunga imekuja baada ya kushinda shindano lililoshirikisha washiriki kutoka nchi 14 na kujinyakulia kitita cha Sh milioni 900, kurekodi nyimbo pamoja na kufanya video chini ya lebo ya Universal Studio ambayo inafanya kazi na wasanii wakubwa duniani.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
579,000SubscribersSubscribe

Latest Articles