25.5 C
Dar es Salaam
Friday, May 3, 2024

Contact us: [email protected]

Sekta ya mawasiliano ya simu inavyoweza kuboresha ubunifu wa kiteknolojia Tanzania

Katika miaka ya hivi karibuni serikali ya Tanzania ikishirikiana na sekta binafsi imechukua hatua mbalimbali kuimarisha uchumi. Nyingi ya juhudi hizi ni sehemu ya mpango wa dira ya kuifanya Tanzania kuwa nchi ya uchumi wakati ya viwanda ifikapo mwaka 2025.
Dira hii inaonyesha mwelekeo wa wapi nchi inakusudia kufika ifikapo mwaka 2025. Moja ya malengo makubwa ya dira hiyo ni kuhakikisha Tanzania inakuwa na uchumi imara, shindani na stahimilivu.
Kuwekeza katika miundombinu ni njia mojawapo ya kuhakikisha lengo linafikiwa. Uwekezaji kwenye eneo kama la reli ya kisasa (SGR) na uboreshaji wa barabara nchini ni moja ya hatua kufanikisha hilo. Miundombinu ya namna hii inaunganisha maeneo mbalimbali nchini na kukuza biashara kwa kuwezesha usafiri bora kwa watu na bidhaa.

Mbali na miundombinu, eneo jingine lenye tija kufikia dira hii ya 2025 ni teknolojia. Watanzania wengi sasa wanazidi kuunganishwa katika dunia ya dijitali hasa kupitia simu zao za mkononi. Wiki chache zilizopota iliripotiwa kwamba zaidi ya wananchi 520,000 katika vijiji 45 nchini ambavyo havikuwa na mtandao wataunganishwa na huduma hiyo. Mradi wa aina hii ni muhimu na unaonyesha namna gani serikali na wadau wa sekta ya mawasiliano wamekusudia kuiunga nchi kidijitali.

Hii ni habari njema. Mfano, Tigo Tanzania imeunda huduma mbalimbali kuhakikisha wateja wake wanafurahia ulimwengu huu wa teknolojia. Huduma hizi ni kama Tigo Pesa na ile ya bima ya afya (m-health) inayowapa wateja nafasi ya kupata bima za afya kwa urahisi.

Huduma hizi zimeleta tija kuja kwa wananchi. Mfano idadi ya watu wasio katika mfumo rasmi wa kifedha nchini imepungua kwa zaidi ya nusu kati ya mwaka 2009 hadi 2017, hasa kutokana na watu kuwa na akaunti za fedha kupitia namba za simu badala ya benki kama ambavyo tulikuwa tumezoea.

Hizi ni hatua njema lakini hata hivyo ili kuendelea kuona kampuni za simu zinabaki kuwa mstari wa mbele kuwezesha Watanzania kufurahia teknolojia, lazima tuendelee kuziunga mkono. Lazima kuendelea kuvutia uwekezaji katika sekta hii na kuweka mazingira ya kisera ambayo yatawezesha ikue zaidi na kuendelea kuwekeza. Hii itasaidia kuongeza fursa kwenye teknolojia na kukuza ubunifu na uzalishaji kwa manufaa ya nchi yetu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles