31.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, September 28, 2021

Menina azindua kampeni ya kusaidia wakina mama na watoto

BEATRICE KAIZA

Staa wa filamu na Bongo Fleva nchini, Menina Abdulkarim ‘Menina’ amezindua kampeni yenye lengo la kuwasaidia wanawake waliojifungua aliyoipa jina la karibu mwanangu.

Akizindua kampeni hiyo leo Jumanne Juni 23, katika Hospitali ya Vijibweni iliyopo Kigamboni jijini Dar es Saalam amewaomba wasanii kusaidia jamii hasa wakinamama na watoto.

Menina amesema wakinamama na watoto waliopo hospitalini wanapitia changamoto nyingi za kiafya na kwamba anafahamu hayo kwakuwa na yeye ni mama pia.

“Ifike wakati vijana na watu mashuhuri kuiona fursa ya kusaidia jamii hasa wakinamama ambao wanapitia changamoto ya kujifungua pamoja na watoto wanaozaliwa na matatizo hasa watoto njiti.

“Kiimani wanasema si vizuri kutoa na kutangaza lakini sisi kama wasanii ninaamini kwa kufanya hivi tunahamasisha wengine ili waweze na wao kufanya hivi,” amesema Menina

Aidha ameongeza kuwa mbali na kutembelea hospitali hiyo na kuwapatia wakinamama zawadi mbalimbali ikiwambo vipima joto, glovu, kiti cha kubebea wagonjwa, mabeseni pamoja na nepi za watoto, ameamua kukarabati chumba cha watoto waliozaliwa kabla ya muda ‘njiti’.

“Watoto wanaozaliwa kabla ya wakati yani njiti wana haki ya kuishi hivyo nimechukua jukumu la kutengeneza chumba cha watoto hao ili waweze kukua vizuri,” amesema.

Pia amesema zoezi hilo la kusaidia wakinamama na watoto litakua endelevu kwa kila hospitali.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
158,612FollowersFollow
519,000SubscribersSubscribe

Latest Articles