Kampeni za Rais Trump zadoda

0
703
Picha hii inaonyesha viti vingi vikiwa wazi, baada ya wafuasi wengi wa Rais wa Marekani, Donald Trump kushindwa kuhudhuria mkutano wa kampeni jijini Oklahoma juzi.

OKLAHOMA, Marekani 

KAMPENI  inayopigania kuchagliwa tena kwa Rais wa Marekani, Donald Trump imepinga madai kampeni ya mitandao ya kijamii kwa njia ya Tik-Tok na K-Pop fans ndizo zilizosababisha kujitokeza kwa idadi ndogo ya watu katika mkutano wa kampeni ya uchaguzi iliyofanyika Oklahoma Jumamosi usiku kuliko ilivyotarajiwa.

Vijana wadogo wanasemekana walijiandikisha kununua tiketi wakiwa na nia ya kutohudhuria mkutano huo kwa lengo la kuhakikisha viti vinabaki tupu.

Lakini kikosi cha kampeni cha 2020 cha Trump 2020, kilisema kilikua kimeondoa tiketi hizo feki.

Kituo cha mkutano huo, maarufu kama The Bank of Oklahoma Center kilichopo eneo la Tulsa ambako mkutano ulifanyika kina viti 19,000.

Ilitarajiwa watu wangejaa hadi nje ya uwanja wa kituo hicho na mipango ikawekwa ili kuhakikisha watu wa ziada wanashiriki kikamilifu tukio hilo, mipango  ilifutwa kutokana na  idadi viti vilibaki wazi.

Kikosi cha zimamoto cha Tulsa kimenukuliwa kikisema zaidi ya viti 6,000 ndivyo vilivyokaliwa katika ukumbi huo, lakini kampeni ya Trump ilisema idadi ya waliohudhuria ilikua ni ya juu zaidi.

Mkurugenzi wa kikosi cha kampeni ya Trump alisema katika taarifa aliyoitoa kuwa “maombi ya tiketi za simu hatukuyafikiria” tuliwapokea watu kwa misingi ya yule anayefika ndiye anayehudumiwa kwanza .

Brad Parscale alivilaumu vyombo vya habari na waandamanaji kwa kuzishawishi familia zisihudhurie kampeni hiyo.

“Watu wa itikadi za mrengo wa kushoto na kampeni za mtandao wanafanya kampeni, wakidhani kwa namna fulani wataathiri mahudhurio ya mkutano wa kampeni, hawajui wanachokizungumzia au namna mikutano ya kampeni inavyofanyika ,” alisema  Parscale.

“Kujisajili kwa mkutano wa kampeni inamaanisha kuwa umethibitisha kuwa utahudhuria kwa namba ya simu na tunatoa mara kwa mara wajumbe gushi, kama tulivyowafanya maelfu katika mkutano wa Tulsa, kwa kuhesabu watu wenye uwezekano wa kuhudhuria.”

Marafiki wa zamani wa Republican walikua wameomba “mamia” ya tiketi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here