24.1 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Scorpion ni nani?

img_0776Na FARAJA MASINDE -DAR ES SALAAM

MTUHUMIWA aliyefikishwa mahakamani akidaiwa kumtoboa macho, Said Mrisho, anayefahamika kwa jina la Salum Henjewele maarufu ‘Scorpion’ ni msanii wa maigizo ya filamu na tamthiliya, MTANZANIA limebaini.

Mbali na usanii, Scorpion alishiriki shindano la ‘Dume Challenge 2012’ na kuibuka mshindi ambapo alijipatia Sh milioni 20 pamoja na mkataba wa kuwa balozi wa mipira wa kiume maarufu ‘dume’.

Taarifa zilizokusanywa na MTANZANIA kwa baadhi ya watu waliowahi kufanyakazi na ‘Scorpion’ zilibainisha kuwa kijana huyo amewahi kushiriki kucheza tamthilia tatu ikiwamo, Red apple, Mirrosos na Thilipina ambayo inaendelea kukamilishwa ambazo zinaandaliwa na Tuesday Kihangala maarufu kama Mr Chusi.

Baadhi ya wasanii aliowahi kushiriki nao katika tamthilia hizo ni pamoja na Mohamed Olotu maarufu kwa jina la Mzee Chilo.

Mzee Chillo ambaye ameshiriki na Scorpion katika tamthiliya ya Thilipina miezi mitatu iliyopita alisema walikutana katika kazi na hamjui undani wake.

“Mimi huyo kijana kwanza hata jina nilikuwa simjui nyie mnaonipigia na kuniuliza ndio mnaofanya nimfahamu.

“Kifupi mimi nilikutana naye miezi mitatu iliyopita ndani ya mwaka huu kwenye tamthiliya lakini nilikuwa simfahamu, hivyo kama utahitaji taarifa zaidi unaweza kuzipata kwa Mr Kihangala, maana hata tamthiliya yenyewe bado haijatoka,” alisema Mzee Chillo.

Kihangala

Akizungumza na MTANZANIA kwa simu, Mr Chusi alisema: “Ni kweli namtambua kijana huyu, namtambua kama kijana mpole sana na anayependa kumcha Mungu kwa kuswali sana pamoja na kufanya mazoezi ya ukakamavu.

“Ni kweli kwamba nimekuwa naye na alikuja kujiunga kwenye Kampuni yangu ya Tuesday mwaka 2010 na kushiriki tamthiliya zangu mbili ambazo ni Mirrosos na Red Apple.

“Baadaye alitoka na kwenda kushiriki kwenye shindano la ‘Dume Challenge’ na akafanikiwa kushinda na kupata mkataba mpaka pale ulipoisha na kurejea tena,” alisema.

Miezi mitatu iliyopita mwaka huu aliomba kushiriki tamthiliya ya Thilipina ambayo bado inaendelea,” alisema Kihangala.

Alisema kabla ya kwenda kushiriki ‘Dume Challenge mwaka 2012’ alikuwa na mkataba tofauti na sasa ambapo hana  mkataba bali anakuja kucheza  vipande vyake na kuondoka.

“Mara nyingi amekuwa ni mtu anayependa sana kufanya mazoezi na ni mwalimu wa karate na amekuwa akiwasisitiza watu kufanya mazoezi na hata kuwa kiongozi tunapokuwa ‘location’,” alisema.

Kihangala aliongeza kuwa katika kufanya kazi pamoja na Scorpion hakuwahi kufahamu makazi yake zaidi ya kukutana ofisini pamoja na mahali wanaporekodi kazi zao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles