27.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, February 8, 2023

Contact us: [email protected]

SBC yachangia madawati 200 yenye thamani ya 22m/- kwa shule ya Gogo

Caption Mkuu wa Wilaya, Sophia Mjema (kushoto) akiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa SBC Ltd Avinash Jha baada ya kukabidhi madawati.
Caption
Mkuu wa Wilaya, Sophia Mjema (kushoto) akiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa SBC Ltd Avinash Jha baada ya kukabidhi madawati.

Kampuni ya SBC Tanzania Limited, watengenezaji wa vinywaji baridi vya PEPSI, imekabidhi madawati 200 yenye thamani ya Shilingi milioni 22, kwa mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema.

Hii ni mwendelezo wa jitihada za kampuni hiyo kuitikia wito wa serikali kuchangia madawati kwa ajili ya kumaliza kabisa matatizo ya madawati mashuleni.

Katika makabidhiano hayo, Mkuu wa Wilaya, Sophia Mjema, aliwashukuru SBC Ltd kwa msaada lakini pia alitoa maagizo kwa watendaji wake kuhakikisha kuwa misaada ya madawati wanayoendelea kupokea kutoka kwa wadau mbalimbali inaelekezwa katika shule mpya na zile za zamani zenye mahitaji.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa SBC, Avinash Jha alisema kuwa kampuni hiyo inatambua changamoto mbalimbali zinazoikumba sekta ya elimu nchini na ndio maana elimu imepewa umuhimu mkubwa katika sera yao ya kuisaidia jamii (yaani Corporate Social Responsibility).

Nae Mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi Gogo, Simon Mdendemi alieleza kuwa shule hiyo mbali na msaada huo wa madawati kutoka katika kampuni ya SBC Tanzania Limited (PEPSI), bado wanayo mahitaji ya kujengewa ofisi ya walimu pamoja na meza 25 na viti 25 vya walimu,” alisema Mwalimu Mdendemi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,871FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles