30.2 C
Dar es Salaam
Sunday, March 26, 2023

Contact us: [email protected]

Sauti Sol wapiga shoo Ikulu ya Obama

SAUTI-SOLNEW YORK, MAREKANI

KUNDI la muziki kutoka nchini Kenya, Sauti Sol, wamefanikiwa kuingia Ikulu ya nchini Marekani na kufanya onyesho la muziki wao kwa Rais Barack Obama.

Wasanii hao walifika Ikulu hiyo kwa mwaliko wa rais huyo, baada ya mazungumzo yao walisimama na kuimba, jambo ambalo lilimnyanyua Obama, akashirikiana na wasanii hao kucheza wimbo waliokuwa wakiuimba.

Wasanii hao wanaweka historia yao ya kuingia ikulu za marais mbalimbali ambapo awali walishaingia Ikulu ya Kenya, walikutana na Rais Uhuru Kenyatta, naye pia walimuimbia.

Wasanii hao bado wapo nchini Marekani kwa ajili ya kazi zao za kimuziki za ushirikiano na mwanamuziki John Legend.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
211,184FollowersFollow
564,000SubscribersSubscribe

Latest Articles