29.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, October 19, 2021

Sarah: ‘Make-up’ huficha ubaya wa sura za wasanii

SARA MAPUNDA (2)NA GEORGE KAYALA

MREMBAJI wa sura za waigizaji wanapokuwa katika harakati za upigaji picha za filamu zao, Sarah Mapunda, amesema kuwa ‘make-up’ husaidia kuficha ubaya wa sura za baadhi ya wasanii wa filamu.

Aliongeza kwamba urembo huwabadilisha wasanii na kuwaweka katika mvuto zaidi ndiyo maana wasiporembwa hushangaza wanapokutana na mashabiki wao kwa kuwa baadhi yao huonekana tofauti na sura zao halisi baada ya kuwafanyia ‘make-ups’.

“Kwa muda mrefu nimekuwa nikiwafanyia make-up wasanii wa filamu ili sura zao ziwe na mvuto wa hali ya juu kwenye kazi zao ndiyo maana wengine wakikutana na mashabiki wao mitaani bila kurembwa hushangaza,” alieleza Sarah.

Baadhi ya wasanii aliowahi kuwafanyia ‘make-up’ na sura zao kuonyesha mvuto wa hali ya juu ni Vicent Kigosi ‘Ray’, Riyama Ally, Halima Yahya ‘Davina, Richie Mtambalike, Jacob Staven ‘JB’, Wema Sepetu, Irene uwoya, Aunt Ezekiel na wengine wengi.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
162,475FollowersFollow
522,000SubscribersSubscribe

Latest Articles