29.2 C
Dar es Salaam
Friday, September 20, 2024

Contact us: [email protected]

Mwigizaji wa Bongo ashinda tuzo Marekani

photoNA CHRISTOPHER MSEKENA

MWIGIZAJI wa filamu nchini, omary Clayton, ameibuka kidedea katika kipengele cha msanii bora wa kiume kwenye tuzo za Califonia Online Viewers Choice Awards (COVCA) zilizotolewa usiku wa kuamkia jana huko Marekani.

Nyota huyo ni moja ya waigizaji wakuu waliofanya vizuri kwenye filamu inayoitwa Dogo Masai iliyomfanya Omary Clayton kuingia kwenye kinyang’anyiro hicho.

“Daah mpaka nimetokwa na machozi, sijui niseme nini ila kikubwa namshukuru Mungu na Watanzania wote kwa kuniunga mkono, hatimaye tuzo imekuja Afrika nairudisha nyumbani Tanzania,” alishukuru Omary.

Tuzo hiyo ilikuwa inawaniwa na wakali kama vile Veron Aldershoff wa Marekani, Dario Merlini wa Ufaransa, Seppe Cosyns wa Ubelgiji na Eric Calderon wa Costa Rica.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles