27.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, May 21, 2024

Contact us: [email protected]

Coast Taarabu kutambulisha Vijukuu wa Tego

TAARABU Khairat Omary na Tariq MohamedNA MWALI IBRAHIM

WAIMBAJI mahiri wa taarabu nchini kutoka kundi la Coast Taarabu, Maua na Omary Tego, wanatarajia kuwatambulisha watoto wao kwenye ulimwengu wa muziki huo katika onyesho lao maalumu litakalofanyika Jumatano katika ukumbi wa Equator Grill, Mtongani Dar es Salaam.

Shoo hiyo inayoitwa ‘Vijukuu wa Tego’ itapambwa na burudani kutoka kwa bendi kongwe ya muziki wa dansi nchini, Msondo Ngoma, Malkia wa Mipasho, Khadija Kopa, Jokha Kassim, Msaga sumu na Dar Modern Taarabu.

Mkurugenzi wa kundi hilo, Omary Tego, alisema usiku huo utaambatana na utambulisho wa nyimbo zao mbili mpya ambapo mashabiki wao watapata nafasi kwa mara ya kwanza kuzisikiliza.

“Sasa tumekuja kivingine tunawaleta watoto wetu nao waonyeshe vipaji vyao walivyojaliwa katika muziki huo, pia mashabiki watapata burudani mbalimbali ikiwa ni pamoja na kusikiliza nyimbo zetu mpya ambazo tumewaandalia kama zawadi kwao,” alisema Maua.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles