33.9 C
Dar es Salaam
Tuesday, February 27, 2024

Contact us: [email protected]

Kim, Kanye West wapata mtoto kabla ya Krismasi

KIM KARDASHIAN and Kanye West Out DinnerLAGOS, NIGERIA

LICHA ya kujitabiria kwamba wangepata mtoto wa pili kipindi cha sikukuu ya Krismasi, mkali wa hip hop, Kanye West na mke wake, Kim Kardashian, wamefanikiwa kupata mtoto wa pili wa kiume juzi.

Kupitia mtandao wa Twitter, Kim aliandika kwamba, “Tulikuwa tunakusubiri kwa muda mrefu, hatimaye muda umefika, karibu sana mwanangu,” aliandika Kim akimkaribisha mdogo wa North West.

Kim pia aliandika katika ‘Website’ yake kwamba, ‘‘Kim Kardashian West na Kanye West wamefanikiwa kupata mtoto wa kiume, mama na mtoto wanaendelea vizuri.”

Mtoto wa kwanza wa Kanye na Kim wa kike alizaliwa mwaka 2013 na mtoto wa kiume amezaliwa mwaka huu 2015 wakitofautiana miaka miwili.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles