24.2 C
Dar es Salaam
Thursday, March 23, 2023

Contact us: [email protected]

Ramsey Nouah kutua Kenya

RAMSEY NUOHNAIROBI, KENYA

MKALI wa filamu nchini Nigeria, Ramsey Nouah, anatarajia kuwasili nchini Kenya kwa ajili ya tamasha la utengenezaji wa filamu bora.

Msanii huyo aliyefanya vizuri kuitangaza tasnia ya filamu ndani na nje ya nchi yao na pia kujijengea upendo mkubwa kwa mashabiki wake hasa wa kike, anatarajiwa kutua nchini humo Desemba 18.

Ramsey Nouah amewataka wapenzi wa filamu nchini humo wajitokeze kwa wingi ili kupata elimu ya filamu itakayoambatana na mashindano ya mitindo mbalimbali.

“Itakuwa siku ya furaha kwangu kukutana na mashabiki wangu nchini Kenya, hii sio siku ya kukosa kwa wale wote wanaonifuatilia watapata nafasi ya kuniuliza chochote moja kwa moja,” aliandika Nouah.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
211,082FollowersFollow
563,000SubscribersSubscribe

Latest Articles