27 C
Dar es Salaam
Saturday, November 26, 2022

Contact us: [email protected]

SANE: SINA TATIZO NA JOACHIM LOW

MANCHESTER, ENGLAND


STAA wa mabingwa wa Ligi Kuu nchini England, Manchester City, Leroy Sane, ameweka wazi kuwa hana tatizo na kocha wa timu ya taifa ya Ujerumani, Joachim Low, baada ya kumwacha kwenye michuano ya Kombe la Dunia.

Mshambuliaji huyo wa pembeni alitikisa vyombo vya habari siku chache kabla ya kuanza kwa Kombe la Dunia nchini Urusi, huku jina lake likiachwa kati ya wachezaji 23 wa timu taifa ambao walikwenda kwenye michuano hiyo, wakati huo Sane aliweza kuipa ubingwa Manchester City na kutwaa uchezaji bora chipukizi na alitoa pasi 15 za mabao na mwenyewe akifunga mabao 10.

Hata hivyo, Ujerumani hawakuweza kufanya vizuri na kujikuta wakitolewa katika hatua ya makundi, lakini mchezaji huyo ameweka wazi kuwa hana tatizo na kocha huyo kutokana na kumwacha na tayari alifanya mazungumzo naye.

“Nilifanya mazungumzo na Joachim Low, bila shaka nilikubaliana na maamuzi yake, alinipa sababu sahihi za kuniacha na ndio maana kila kitu kipo sawa na wala sina tatizo naye.

“Nilijisikia vibaya baada ya kuona wanatolewa kwenye hatua ya makundi, najua ni jambo ambalo liliwaumiza wengi,” alisema Sane.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
205,558FollowersFollow
557,000SubscribersSubscribe

Latest Articles