24.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 18, 2024

Contact us: [email protected]

MBUNGE AVULIWA UDIWANI KWA KUTOHUDHURIA VIKAO

                                                               |Suzan Uhinga, Tanga


Mkurugenzi wa Jiji la Tanga, Daudi Mayeji ametangaza Kata ya Ngamiani Kusini kuwa wazi  kutokana na Diwani wake ambaye pia ni Mbunge wa Tanga Mjini, Mussa Mbaruku (CUF), kutohudhuria vikao zaidi ya sita vya Baraza la Madiwani.

Akizungumza na Mtanzania Digital, leo Jumatatu Julai 23, Mayeji amesema mbunge huyo amepoteza sifa kwa mujibu wa Sheria ya Mamlaka za Majiji.

“Sheria ya Serikali za Mitaa, Mamlaka ya Majiji Sura ya 228, kifungu cha 30B ndiyo imemuondoa, ni kwa mujibu wa sheria,” amesema Mayeji.

Mbaruku aligombea nafasi hizo za ubunge na udiwani katika chaguzi Mkuu mwaka 2015, kupitia Chama cha Wananchi (CUF) na kushinda zote.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles