24.4 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 23, 2024

Contact us: [email protected]

CHELSEA WAIGEUKA MADRID KWA HAZARD

LONDON, ENGLAND


Uongozi wa klabu ya Chelsea, umeigeuka Real Madrid katika mipango ya kutaka kumsajili mshambuliaji wa timu hiyo, Eden Hazard, katika kipindi hiki cha majira ya joto.

Siku za hivi karibuni viongozi wa timu hizo walikutana na kufikia makubaliano ya awali, lakini juzi jioni Chelsea wamebadili mipango hiyo na kusema hawapo tayari kumwacha mchezaji huyo akiondoka kwa dau lolote lile.

Kocha mpya wa Chelsea, Maurizio Sarri, amesisitiza kuwa yupo kwenye mipango ya kumtumia mchezaji huyo msimu mpya wa ligi, hivyo hawawezi kumwacha akiondoka.

Hata hivyo, Hazard alikataa kuongeza mkataba ndani ya Chelsea ambao ulimtaka achukue kiasi cha pauni 300,000 kwa wiki, lakini Chelsea wanaamini mchezaji huyo hawezi kutua Santiago Bernabeu.

Real Madrid wametenga kiasi cha pauni milioni 150 kwa ajili ya kumsajili mchezaji huyo baada ya mshambuliaji wake hatari, Cristiano Ronaldo, kujiunga na klabu ya Juventus kwa uhamisho wa pauni milioni 100.

Hata hivyo, Hazard bado ana mkataba na klabu yake hiyo ya Chelsea hadi mwaka 2020. Kocha wa timu ya taifa ya Ubelgiji, Roberto Martinez, mara baada ya kumalizika kwa michuano ya Kombe la Dunia nchini Urusi, alimtaka mchezaji huyo kufanya maamuzi ya kuondoka Chelsea ili aweze kupata changamoto nyingine.

Hadi sasa mchezaji huyo hajajiunga na kikosi cha Chelsea ambacho kipo nchini Australia kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya, bado yupo nchini Hispania kwenye mapumziko baada ya kumalizika kwa Kombe la Dunia, huku timu yake ya Ubelgiji ikishika nafasi ya tatu kwenye michuano hiyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles