23.3 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Samuel Sitta apelekwa ujerumani kutibiwa

Rais Dk. John Magufuli (kulia), alipokwenda kumjulia hali Samuel Sitta hivi karibuni.
Rais Dk. John Magufuli (kulia), alipokwenda kumjulia hali Samuel Sitta hivi karibuni.

Na Kulwa Karedia,

HALI ya afya ya Spika mstaafu, Samuel Sitta si nzuri,baada ya Serikali kumpeleka nchini Ujerumani kwa matibabu zaidi.

Habari za uhakika ambazo MTANANIA imezipita jijini Dar es Salaam jana, zinasema Sitta alipelekwa Ujerumani juzi kwa matibabu baada ya afya yake kubadilika ghafla.

“Nilimtembelea siku moja kabla ya kupelekwa nje ya nchi, kwa kweli hali ya afya yake ilikuwa imedhoofu, namwombea Mungu amsaidia apone haraka ili arudi kuendelea na majukumu yake.

“Nimesikitishwa mno na taarifa za kuzushiwa kifo mzee wangu huyu, Mungu ni mwema najua bado anampigania uhai wake…hii tabia ya mitandao ya kijamii kumzushia mtu kifo sijui inafaidika nini.

“Mpaka anaondoka nchini kwenda matibabu natambua amekuwa asikumbuliwa mno na tatizo la miguu, sasa mimi si daktari wake siwezi kuongeza zaidi,”kilisema chanzo chetu.

Septemba 19, mwaka huu, Rais Dk. John Magufuli alimtembelea Sitta hospitalini alikolazwa kwa muda sasa kumjulia hali, kisha kumwombea dua Mungu amsaidie.

Siku iliyofuata Waziri Mkuu,  Kassim Majaliwa naye alimtembelea hospitalini kumjulia hali.

Sitta ameshika  nyadhifa mbalimbali, zikiwamo za Spika wa Bunge kuanzia mwaka 2005 hadi 2010, uwaziri na ubunge kwa kipindi kirefu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles