31.2 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

Wadau wajadili muswada sheria ya huduma za habari

Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri(TEF), Theophil Makunga.
Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri(TEF), Theophil Makunga.

Na MAULI MUYENJWA, DAR  ES SALAAM

WADAU wa habari nchini wameanza kujadili muswada wa sheria ya huduma za habari wa mwaka 2016.

Akizungumza na waandishi wa habari   Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri(TEF), Theophil Makunga alisema  kutokana na umuhimu wa sheria inayotungwa umeonekana umuhimu wa kupanua wigo wa kukusanya maoni.

Alisema  taasisi mbalimbali za habari na wadau wa habari wamekwisha kuanza kutekeleza wajibu huo  Dar es Salaam, lakini pia wameweka mpango utakaowezesha kukusanya maoni ya watu wengine kutoka mikoa mbalimbali nchini.

“Maoni haya yatakusanywa kupitia klabu za waandishi wa habari ambazo zimesambaa nchi nzima.

“Kupitia kwa viongozi wao na tunaamini waandishi wa habari na wadau wengine wa habari watasoma muswada huo, kufanya uchambuzi wa maudhui yake na kutoa maoni yatakayowezesha kupatikana sheria bora,” alisema.

Makunga alisema  muswada huo si mali ya wamiliki wa vyombo vya habari, wahariri au vyumba vya habari  vya Dar es Salaam pekee bali unagusa maslahi mapana ya sekta nzima ya habari nchini.

“Sheria inayokusudiwa kutungwa inaweza kutumika miaka 50 ijayo au zaidi kama ilivyo kwa sheria ya magazeti ya 1976 ambayo imekuwapo kwa miaka 40 sasa hivyo ni muhimu kushirikisha wadau   iwe bora zaidi,”alisema.

Katibu wa TEF, Nevile Meena, alisema   kuna changamoto ya muda katika suala hilo lakini watajitahidi kadri inavyowezekana kuwafikia wadau wa habari watoe ushiriki wao katika muswada huo.

“Kwa taarifa hii tunawaomba waandishi wa habari kote nchini na wadau wa habari kutumia fursa hii  kuwezesha upatikanaji wa maoni yatakayosaidia itungwe sheria bora kwa maslahi ya nchi,  sekta ya habari na taifa kwa ujumla,” alisema Meena.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles