23.4 C
Dar es Salaam
Saturday, April 27, 2024

Contact us: [email protected]

Samia mgeni rasmi maonyesho ya bidhaa za viwandani

Na GUSTAPHU HAULE-PWANI

MAKAMU wa Rais, Samia Suluhu Hassan, anatarajia kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa maonyesho ya bidhaa za viwandani yanayoanza leo Kibaha mkoani Pwani.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Evarist Ndikilo, alisema maonyesho hayo ya siku saba yatahusisha wawekezaji mbalimbali kutoka ndani na nje ya Mkoa wa Pwani.

Ndikilo, alisema maonyesho hayo yataambatana na kongamano kubwa la wawekezaji ambalo litafanyika Oktoba 19 na litazinduliwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.

Alibainisha maonyesho hayo yanalenga kuonyesha namna ambavyo mkoa unatekeleza juhudi za ujenzi wa viwanda na uzalishaji wa bidhaa zake kuelekea uchumi wa kati.

Ndikilo alisema kongamano hilo linafanyika ikiwa ni utekelezaji wa maagizo ya Waziri Mkuu kwa kila mkoa kufanya kongamano, lakini hata hivyo yatafungwa Oktoba 23 na Waziri Mkuu mstaafu Mizengo Pinda.

“Maonyesho haya ni  fursa kwa wazalishaji wa bidhaa kuonyesha bidhaa zao ili ziweze kupata soko kwa watakaotembelea, lakini pia kongamano litafungua na kuonyesha fursa zilizopo Mkoa wa Pwani,” alisema Ndikilo.

Alisema hadi sasa maandalizi yapo vizuri na tayari  washiriki 206 wamethibitisha kushiriki, pamoja na taasisi wezeshi mbalimbali na taasisi za huduma za benki.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles