31.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, December 10, 2024

Contact us: [email protected]

TMA yatoa tahadhari mvua kubwa siku mbili

Na MWANDISHI WETU-DAR ES SALAAM

MAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), imetoa angalizo kuhusu mvua kubwa ya vipindi vifupi inayotarajiwa kunyesha kwa siku mbili katika mikoa ya Pwani ya Bahari ya Hindi, inayotarajiwa kuanza leo hadi kesho.

Taarifa ya Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Agnes Kijazi, ilieleza jana kuwa mvua hiyo kubwa inaratajiwa kunyesha katika mikoa ya Dar es Salaam, Pwani, Tanga, visiwa vya Unguja na Pemba pamoja na kaskazini mwa Mkoa wa Morogoro.

Ilieleza kwamba kuwepo kwa uwezekano wa kutokea kwa mvua hizo ni wa wastani na hata kiwango cha athari zinazoweza kutokea ni cha wastani pia.

 “Baadhi ya makazi yataweza kuzungukwa na maji, ucheleweshwaji wa usafiri, kusimama kwa muda kwa baadhi ya shughuli za kiuchumi na kijamii,” inasomeka sehemu ya taarifa hiyo.

Hata hivyo, wananchi wanashauriwa kuendelea kufuatilia taarifa za utabiri kutoka TMA na kuzingatia tahadhari zilizotolewa na marejeo yake pamoja na kupata na kuzingatia ushauri na miongozo ya wataalamu katika sekta husika ili kupunguza athari zinazoweza kujitokeza.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, katika baadhi ya maeneo hali hiyo inaweza kubadilika, hivyo TMA itaendeela kutoa taarifa za mara kwa mara iwapo kutakuwa na mabadiliko ya aina yoyote.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles