26.9 C
Dar es Salaam
Monday, December 9, 2024

Contact us: [email protected]

SAMATTA AINUSURU GENK ISILIZWE

Na MWANDISHI WETU

MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Samatta, ameuanza msimu mpya wa Ligi Kuu ya Ubelgiji na moto baada ya kuiokoa timu yake ya Genk na kipigo na kulazimisha sare ya mabao 3-3 dhidi ya Waasland-Beveren.

Katika mchezo huu uliopigwa juzi kwenye Uwanja wa Luminus Arena, jijini Genk, Samatta aliifungia bao la kusawazisha dakika ya 80 huku pia akitoa pasi moja iliyozaa bao.

Waasland-Beveren waliuanza mchezo kwa kasi na kufanikiwa kwenda mapumziko wakiwa mbele kwa mabao 2-0, yaliyofungwa na Olivier Myny dakika 45 na Zihno Gano dakika ya 47.

Lakini Genk walizinduka na kukomboa mabao hayo kupitia kwa Jose Naranjo dakika ya 70, na Samatta dakika ya 80 kabla ya Mtanzania huyo kumsetia Siebe Schrijvers aliyefunga la tatu dakika ya 82.

Genk ikidhani imemaliza kazi katika mchezo huo na kuoondoka na pointi tatu, Zinho Gano alifanya yake kwa mara nyingine baada ya kuisawazishia Waasland-Beveren kwa kufunga bao la tatu dakika ya 90.

Mchezo huo ulikuwa wa 56 kwa Samatta tangu Januari mwaka jana alipojiunga na Genk akitokea TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).

Kati ya michezo 56, 34 ameanza na 21 ametokea benchi.

Mshambuliaji huyo wa zamani wa Simba na African Lyon, amefanikiwa kufunga jumla ya mabao 19 tangu alipojiunga na Genk huku akionyeshwa kadi za njano mara nne.

Genk itashuka tena uwanjani Agosti 4, kuwakabili Standrd Liege katika mchezo wa Ligi Kuu ya nchini Ubelgiji.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles