23.2 C
Dar es Salaam
Saturday, July 27, 2024

Contact us: [email protected]

ALVES AINGIA KWENYE HISTORIA YA MATAJI

PARIS, UFARANSA

BEKI mpya wa klabu ya PSG, Dani Alves, ameingia kwenye historia ya wachezaji waliotwaa mataji mengi duniani baada ya juzi kuongeza taji la 34 akiwa na klabu hiyo mpya.

PSG juzi ilishuka dimbani dhidi ya wapinzani wao Monaco na kufanikiwa kushinda mabao 2-1 katika mchezo wa kuwania taji la French Super Cup, beki huyo alifunga bao moja katika ushindi huo.

Alves amejiunga na klabu hiyo katika kipindi hiki cha majira ya joto akitokea klabu ya Juventus ya Italia na huku aliitumikia klabu hiyo msimu mmoja na kutwaa jumla ya mataji matatu ikiwa pamoja na lile la Ligi Kuu.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 34, alikuwa anahusishwa kutaka kujiunga na klabu ya Manchester City kwa mkataba wa miaka miwili na ilidaiwa kwamba tayari alikuwa amemalizana na kocha wa timu hiyo Pep Guardiola, lakini alishangaza mashabiki baada ya kuonekana mjini Paris akiwa ndani ya klabu ya PSG.

Hata hivyo, baada ya kujiunga na klabu hiyo ya PSG, Alves aliomba radhi kwa Pep Guardiola na mashabiki wa Manchester City kutokana na usumbufu aliowapa na alisema kuwa amefanya maamuzi hayo ya kujiunga na PSG kwa ajili ya kwenda kutwaa mataji.

Tayari amefanikiwa kuanza na taji ikiwa ni mchezo wake wa kwanza wa kuwania taji tangu ajiunge mapema mwezi huu, taji hilo la French Super Cup linamfanya awe kwenye orodha ya wachezaji watatu duniani ambao wamechukua mataji mengi.

Alves anashika nafasi ya tatu, huku nafasi ya kwanza ikichukuliwa na nyota wa zamani wa timu ya Taifa ya Brazil, klabu ya Barcelona na PSG, Maxwell Andrade mwenye mataji 36, akifuatiwa na Ryan Giggs mwenye mataji 35.

Alves mwenye mataji 34 kuna uwezekano wa kuongeza mataji zaidi ya hapo kutokana na uwezo alionao na klabu anayoitumikia, hivyo endapo msimu mpya wa ligi PSG ikifanikiwa kutwaa mataji zaidi ya mawili beki huyo ataweka historia ya aina yake.

Nafasi ya nne inachukuliwa na mshambuliaji wa klabu ya Manchester United, Zlatan Ibrahimovic, akiwa na mataji 33.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles