22.1 C
Dar es Salaam
Monday, July 22, 2024

Contact us: [email protected]

Safari za ndege zarejea Hong Kong

HONG KONG

UWANJA wa ndege wa Hong Kong umeanza kutoa huduma za usafiri wa ndege baada ya sintofahamu  iliyoshuhudia maofisa wa polisi wakipambana na waandamanaji.

Mamia ya safari za ndege zilisitishwa siku ya Jumanne baada ya waandamanaji kufurika katika majengo ya kiwanja cha ndege.

Mapema jana ndege zilionekana kuanza safari zake kama ilivyopangwa, ingawa kulikuwa na baadhi ambazo zilikuwa ama zimesitisha safari au zimechelewa.

Baada ya siku kadhaa za kadhia, Mamlaka ya Uwanja wa Ndege  ilisema kuwa imechukua kibali cha muda kuzuia waandamanaji kuijngia katika maeneo fulani fulani.

Hatua za kiusalama pia zilichukuliwa hasa katika eneo linaloendesha shughuli za uwanja wa ndege na wafanyakazi pamoja na abiria ndio walioruhusiwa kupita wakiwa na vitambulisho.

Maandamano hayo yameingia wiki ya kumi tangu waandamanaji waanze kuipinga serikali.

Uwanja wa ndege ambao waandamanaji hao waliuvamia ni moja ya viwanja ambavyo vinatumika sana duniani.

Waandamanaji waliufanya uwanja huo wa ndege kama eneo lao la kupaza sauti nje ya mipaka ya Hong Kong tangu Ijumaa ya wiki iliyopita na maandamano yao yalikuwa ya amani.

Jumanne waandamanaji walizuia wasafiri kupata huduma za ndege, wakitumia toroli za kubeba mizigo kuweka vizuizi huku wao wakiwa wamekaa chini.

Baadhi ya waandamanaji walikuwa wamebeba mabango yenye alama ya kuomba msamaha abiria kwa sababu ya usumbufu uliosababishwa na maandamano yao.

Hata hivyo mambo yalibadilika ghafla baada ya mwanaume mmoja anayedaiwa kuwa ni ofisa wa polisi aliyekuwa katika kundi la waandamanaji hao kudaiwa kupandikizwa.

Hali hiyo ilisababisha polisi kuingia uwanjani hapo na kuanza kupambana na

waandamanaji.

Hata hivyo waandamanaji walimdhibiti kwenye kona na baada ya kuanguka chini alichukuliwa na maofisa wenzake.

Katika video moja inaonyesha, polisi kwa hasira akichukua bunduki yake baada ya kujeruhiwa na fimbo aliyokuwa ameibeba wakati akimsukuma mwanamke mmoja.

Wanaume wengine wawili  ambao pia walishukiwa kuwa maofisa wa polisi nao walijikuta katika mabishano makali na waandamanaji

Vitendo hivyo vimekuja baada ya polisi kukiri Jumatatu kwamba kuna maofisa ambao wamepandikizwa katikati ya waandamanaji.

Msingi wa maandamano hayo ni muswada ambao Hong Kong inataka kuupitisha na kuwa sheria wa kutaka raia wa eneo hilo kushitakiwa China.

Pamoja na hayo maandamano hayo ambayo yameingia wiki ya kumi yamezaa madai megine ikiwamo kutaka utawala wa demokrasia, kuitishwa kwa uchaguzi na kumwondoa kiongozi wa sasa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles