31.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Mama, mtoto waliopona Ebola waungana na familia zao

GOMA, CONGO

WAATHIRIKA wawili wa Ebola nchini Congo wameungana na familia zao baada ya kupona ugonjwa huo.

Wanasayansi wana matumaini muda si mrefu Ebola inaweza kuzuilika au kutibika baada majaribio ya dawa mbili kuonyesha mafanikio ya kutibu ugonjwa huo.

Watafiti wanasema katika matibabu ya awali zaidi ya asilimia 90 ya watu walioathirika na ugonjwa huo wanaweza kupona iwapo watapewa  dawa aina ya REGN-EB3 na mAb114.

Dawa hizo mbili zilibainika kutibu ugonjwa huo kwa kutumia mifumo ya kinga iliyovunwa kutoka kwa mwathirika wa Ebola.

Majaribio yake yalifanywa kwa uratibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) ambalo jopo lake limependekeza matibabu hayo kutumiwa kwa wagonjwa wote.

Dawa hizo zinafanya kazi ya kushambulia virusi vya Ebola kwenye kinga ya mwili, na kuweka sawa seli.

Kwa mujibu wa Daktari, Sabue Mulangu, majaribio ya dawa hizo mbili yanaweza kushuhudia asilimia 60  ya wagonjwa 681 wanapona.

Watu hao wawili ambao wamepona Ebola kwa kutumia njia hiyo iliyogunduliwa wameruhusiwa kutoka ktika kituo cha matibabu huko mashariki ya Congo na kuungana na familia zao.

Watu hao wawili ni miongoni mwa kundi la watu wanne waliokuwa wameathirika na ugonjwa huo Goma, jiji kubwa lililoathirika na ugonjwa huo ambao hadi sasa umeua watu 1,800.

Watu  wengine wawili katika kundi hilo walikufa kwa ugonjwa huo.

Walionusurika au kupona ni mjane na mtoto wa mwanaume aliyefariki baada ya kuambukizwa ugonjwa huo.

Ugonjwa huo ulilipuka Congo  mwezi Agosti mwaka jana ukiingia kwenye nafasi ya 10 kwa kuwa na maambukizi mengi tangu virusi vya ugonjwa huo vigundulike mwaka 1976.

Ugonjwa huo uliwahi kuathiri vibaya Afrika Magharibi kati ya 2014-16, ambako watu takribni 28,616 waliathirika, wengi wao wakiwa ni raia kutoka Guinea, Liberia na Sierra Leone.

Idadi kubwa iliyorekodiwa ya watu waliokufa kwa ugonjwa huo ni ile iliyofikia 11,310

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles