24.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

SADC –DFI KUJADILI PAMOJA UCHUMI WA VIWANDA

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi za Maendeleo ya Fedha   katika SADC -DFRC, Stuart Kufeni

Na ASHA BANI-DAR ES SALAAM

WAKUU wa Mtandao wa Taasisi za Maendeleo ya Fedha wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC-DFI) wamedhamiria kuharakisha maendeleo ya viwanda katika nchi mwanachama wa jumuiya hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi za Maendeleo ya Fedha   katika SADC -DFRC, Stuart Kufeni, alisema hiyo ni fursa ya pekee katika kukuza uchumi wa viwanda na hata kuongeza ajira katika nchi hizo.

Alisema nchi za Kusini mwa Afrika zote zina utajiri mkubwa kutokana na rasilimali zake, hasa za madini.

“Hii ni kwa kutambua kipaumbele cha umuhimu wa viwanda kilichowekwa na wakuu wa SADC kama silaha muhimu ya kuelekea kufanikiwa ukuaji endelevu wa uchumi na maendeleo katika eneo la SADC na kuchochea ustawi wa watu wake,’’ alisema Kufeni.

Alisema mafanikio ya utekelezaji wa mkakati na mpango wa uendelezaji wa viwanda wa eneo la SADC utahitaji uwekezaji mkubwa katika sekta mbalimbali za viwanda.

Kufeni alisema kwa sababu hiyo taasisi za fedha, hasa DFIs kwa ushirikiano na sekta binafsi, zitashiriki kwa ukamilifu katika kukusanya nguvu ya upatikanaji wa rasilimali fedha.

Alisema jukwaa litaangalia wajibu na uzoefu wa FDIs katika kusaidia maendeleo ya viwanda kutokana na ushiriki wao katika ngazi ya kanda na taifa kama gurudumu la kusukuma ajenda ya viwanda kama silaha ya ukuaji wa uchumi.

“Kwamba kuna umuhimu wa DFIs kuchukua jukumu kuu la upatikanaji wa rasilimali fedha kuhakikisha kufikia malengo ya maendeleo ya taifa na kanda chini ya Mpango Mkakati Elekezi wa Maendeleo wa SADC (2015-2020),’’ alieleza Kufeni.

Hata hivyo taasisi za maendeleo DFIs, ikiwa ni pamoja na Benki ya Maendeleo ya Uwekezaji TIB, Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC) na Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania zitakuwa wenyeji wa mkutano wa siku mbili wa nusu mwaka wa Mtandao wa Taasisi za Maendeleo ya Fedha wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC-DFI) unaotarajiwa kuanza Dar es Salaam kesho.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles