RAIS WA ZAMBIA ATANGAZA HALI YA DHARURA

Rais wa Zambia Edgar Lungu ametangaza hali ya dharura nchini humo kutokana na moto mkubwa uliyotekteza soko kuu la mjini Lusaka.

Moto huo pamoja na visa vingine kama hivyo unadhaniwa kuanzishwa kwa maksudi na rais Lungu anasema ni vitendo vya kuhujumu uchumi ili kuifanya Zambia isitawalike vyema.

Hata hivyo wapinzani wake wanasema Rais Lungu anatumia mikasa hiyo kama kisingizio cha kuendeleza utawala wake.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here