23.3 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

‘Sabasaba ya mwaka huu ni ya kipekee’-Wadau

Na Esther Mnyika, Mtanzania Digital

Wadau wa Maonyesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa (DITF) maarufu kama Sabasaba wamesema maonyesho ya mwaka huu ni ya kipee kwa kuwa yanatoa fursa kwa Taasisi, kampuni wajasiriamali na watu mbalimbali kwa kuwa wanashirikishwa na Tantrade katika maandalizi ya maonyesho hayo, hivyo wanatarajia mauzo kuongezeka.

Akizungumza leo Juni 2, jijini Dar es Salaam na waandishi wa habari Mkurugenzi wa Kampuni Tanzakwanza Stragists, Francis Daudi amesema wana mabanda maalum Expo Village lengo likiwa ni kuonyesha huduma zinazopatikana nchini

“Kampuni yetu kwa kushirikiana na TanTrade banda maalum expovillage imelenga kukutanisha sekta nane ambazo ni madini, kilimo, mazingira, uwekezaji michezo na zingine kujadili changamoto na fursa zilizopo kwenye mabanda maalum,”amesema Francis.

Amesema maonyesho hayo ni kuwavutia wawekezaji wa ndani na nje na kuonyesha rasilimali watu iliyopo nchini.

Naye Mtafiti na Mgunduzi wa vyakula vya asili kutoka kampuni ya Dorikin, Profesa Dorcas Kibona amesema kilimo ndo kila kitu, ni uhai, na kiiunua mgongo wa uchumi.

Amesema kampuni hiyo imejikita kwenye kufanya utafiti wa vyakula vya asili na lengo ni kufanya uwekezaji wa chakula nchini.

“Kampuni hii imefanya vizuri kwenye maonyesho ya chakula Italia na tunaendelea kufanya vizuri ili wawekezaji wafuate nchini na wanunue kwa dola na vijana tupende kilimo,”amesema Prof. Dorcas.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Machinga Mkoa wa Dar es Salaam, Namoto Yusuph amesema wanataka kuwa na kituo maalum cha pamoja cha kuzalisha bidhaa.

“Kuna machinga wengi ni wazalishaji wa bidhaa kama batiki, sandozi na bidhaa mbalimbali tunahitaji kuwa na kituo maalum ili iwe rahisi kuwaunganisha na wataalamu namna ya kutengeneza bidhaa zenye viwango na Mamlaka ya Viwango Tanzania(TBS) ikague bidhaa hizo,”amesema Yusuph huku akiwaomba machinga kujitokeza kwa wingi kwenye maonyesho ya sabasaba.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles