24.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, September 10, 2024

Contact us: [email protected]

Sababu za kukataliwa Naibu Spika na wapinzani

tuliaKhamis Mkotya na Aziza Masoud, Dodoma

KAMBI Rasmi ya Upinzani Bungeni imeeleza sababu sita zilizoisukuma kambi hiyo kuwasilisha ofisini kwa Spika, taarifa ya kusudio la kupeleka bungeni hoja ya kumwondoa madarakani Naibu Spika, Dk. Tulia Ackson.

Akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za Bunge jana, mwakilishi wa wabunge wa kambi hiyo, James ole Millya, alisema tangu ameanza kuliongoza Bunge, Dk. Tulia ameonyesha udhaifu mkubwa, ndiyo maana kambi hiyo inataka kiongozi huyo aondolewe kwa azimio la Bunge.

Millya ambaye ni Mbunge wa Simanjiro (Chadema), alisema pamoja na mambo mengine, Naibu Spika amevunja kanuni ya 8 (b) inayokataza upendeleo na kanuni ya 5 (1) inayomtaka Spika kuzingatia mila na desturi na uamuzi wa maspika wa mabunge mengine.

Millya alisema hoja yao imejikita katika kanuni ya 138 (1) inayosema: “Utaratibu wa kumwondoa madarakani Naibu Spika chini ya Ibara ya 85 (4) (c) ya Katiba utakuwa kama ule wa kumwondoa Spika, ispokuwa tu taarifa ya kusudio la kumwondoa Naibu Spika madarakani inayoeleza sababu kamili za kuleta hoja hiyo  itapelekwa kwa Spika ambaye ataiwasilisha kwenye Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kwa ajili ya kujadili,” alinukuu.

Millya ambaye aliongozana na Mbunge wa Viti Maalumu, Riziki Shaali Mngwali (CUF), alieleza sababu hizo kama ifuatavyo:

“Naibu Spika wa Bunge, Dk. Tulia Ackson ameweka mbele maslahi ya chama chake cha siasa kuliko maslahi ya Bunge kinyume na kanuni ya 8 (b) ya Kanuni za Kudumu za Bunge.

“Tarehe 6 Mei, 2016 Naibu Spika alitumia vibaya madaraka ya kiti cha Spika kwa kutoa uamuzi wa mwongozo ambao ulikua unakiuka ibara ya 12 (2) ya Katiba isemayo kuwa; “Kila mtu anastahili heshima ya kutambuliwa na kuthaminiwa utu wake” mwongozo uliokuwa unapinga udhalilishaji wa wanawake.

“Tarehe 28 Aprili, 2016 Naibu Spika alivunja kanuni ya 64 (1) zinazokataza mbunge kutumia lugha ya matusi kwa mbunge au mtu mwingine yeyote na kukataza matumizi ya lugha ya kuudhi au kudhalilisha watu wengine, ambako Naibu Spika alinukuliwa akisema: “Mheshimiwa Bwege, usionyeshe ubwege wako humu ndani…”

“Tarehe 30 Mei, 2016 Naibu Spika aliamua kwa makusudi kuvunja ibara ya 63 (2) ya Katiba kwa kutumia vibaya kanuni ya 69 (2) na 47 (4) ya kanuni za kudumu kumhusisha mh Joshua Nassari kwa upande mmoja na Bunge zima kwa upande wa pili kutimiza majukumu yake ya kikatiba ya kuisimamia na kuishauri Serikali,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles