24.4 C
Dar es Salaam
Wednesday, June 19, 2024

Contact us: [email protected]

Mikataba ya madini kupitiwa upya  

madini.NA HADIA KHAMIS, DAR ES SALAAM

MWENYEKITI wa Bodi ya Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), , amesema atahakikisha shirika hilo linapitia upya mikataba ya wabia wa madini ili kuondokana na mikataba mibovu isiyokuwa na tija.

Balozi Muganda aliyasema hayo jana alipokuwa akizindua Bodi ya Wakurugenzi ya shirika hilo Dar es Salaam na kuongeza kuwa Stamico inakabiliwa na changamoto kubwa ya miradi kushindwa kusimamiwa vyema.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Profesa Justin Ntalikwa, alimuagiza Balozi Muganda kuhakikisha anafuatilia miradi yote inayomilikiwa na shirika hilo.

Profesa Ntalikwa alisema  ili shirika hilo liweze kufanikisha mipango ya Serikali ni lazima miradi inayomilikiwa na shirika ikasimamiwa ipasavyo.

Alisema sera ya madini ya mwaka 2009 inasisitiza ongezeko la ushiriki wa Serikali na wananchi katika shughuli za madini ili kuongeza manufaa yatokanayo na madini.

“Kutokana na mtazamo huo wa Serikali Stamico imepewa jukumu la kushiriki katika uwekezaji kwenye sekta ya madini kwa niaba ya Serikali, hivyo bodi bado ina wajibu mkubwa wa kulisimamia hili kwa manufaa ya taifa,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles