24.8 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

SABABU ZA KUFUNGWA VYUO VITANO VYA UFUNDI ZAELEZWA

NA RAMASHANI HASSAN, DODOMA

SERIKALI imesema upungufu wa watumishi ulisababisha kufungwa  vyuo vitano vya ufundi kwa ajili ya watu wenye ulemavu.

Kauli hiyo iliitoa bungeni Dodoma jana na  NAIBU Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira na Vijana, Antony Mavunde wakati akijibu  swali la msingi la  Mbunge wa Viti Maalum (Chadema), Dk. Elly Macha.

Dk. Macha alihoji: ‘’Ni sababu gani zilizosababisha vyuo hivyo vitano vifungwe wakati kuna mahitaji makubwa ya watu wenye ulemavu kupata mafunzo ya ufundi.’’

 “Je, serikali ina mpango gani wa kufungua haraka vyuo  vilivyofungwa ili viendelee kutoa mafunzo ya ufundi kwa watu wenye ulemavu … serikali ina mkakati gani wa kujumuisha watu wenye ulemavu kwenye vyuo vyake vya VETA na FDC?”

 Akijibu, Mavunde alizitaja sababu hizo kuwa ni upungufu wa watumishi  na baadhi yao kustaafu na wengine kufariki dunia.

 Alisema serikali ina nia ya dhati ya kuhakikisha  watu wenye ulemavu nchini wanapata mafunzo siyo tu ya ufundi, bali ya aina nyingine yatakayokidhi mahitaji ya ajira na kuondoa utegemezi kwa watu wenye ulemavu.

Pia alisema serikali imewasilisha maombi maalum Hazina ya kuomba fedha za maendeleo kwa mwaka wa fedha 2017/18 ambazo   zitatumika kufanya ukarabati na kuboresha miundombinu ya vyuo mbalimbali nchini.

“Vilevile, wizara imewasilisha IKAMA ya watumishi  utaratibu wa kuajiri watumishi ufanyike mapema kuziba nafasi zilizo wazi,”alisema Mavunde

   Naibu waziri alisema mkakati wa serikali ni kuwa na walimu wenye mbinu za kufundisha watu wenye ulemavu katika kozi ya ualimu MVTTC ambayo ipo Monduli inayohusu mbinu za kufundisha watu wenye ulemavu.

 Alisema pia lengo la Serikali ni kukarabati miundombinu ya njia za kutembelea na majengo  kuwapa fursa watu hao kushiriki katika mafunzo ya ufundi bila kikwazo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles