26.4 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 6, 2023

Contact us: [email protected]

NI KOSA KUTOPOKEA MALIPO KWA SHILINGI

Na RAMADHAN HASSAN-DODOMA

WAZIRI wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango, amesema ni kosa kisheria kwa mtu yeyote kukataa kupoke fedha inayotumia shilingi ya Tanzania katika malipo yoyote nchini.
Dk.Mpango alitoa kauli hiyo bungeni jana alipokuwa akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Baraza la Wawakilishi, Jaku Hashim Ayoub (CCM).

Jaku alihoji: ‘’Nini kauli ya serikali kuhusiana na shule binafsi zinazotoza fedha za malipo mbalimbali kwa dola na kukataa kupokea shilingi ya Tanzania huku zikijua ni kosa’’
Akijibu, Dk Mpango alisema Sheria ya Usimamizi wa Fedha za Kigeni ya Mwaka 1992 inamruhusu mtu yoyote kupokea na kutumia fedha za kigeni katika kukuza uchumi wa nchi, hivyo kutumia fedha hizo siyo kosa.

“Kosa linakuja mtu anapokataa kupokea malipo kwa fedha ya shilingi ya kitanzania,” alisema.

Alisema kwa mujibu wa  sheria hiyo, watanzania wanatakiwa kutoa taarifa mara moja kwa mamlaka husika   hatua za sheria zichukuliwe dhidi ya mtu aliyekataa kupokea fedha za malipo kwa shilingi ya Tanzania.

 Mbunge huyo katika swali la nyongeza, alitaka kujua kama serikali inatambua kuwa kuna tatizo kwa kulipishwa ada ya masomo kwa fedha za kigeni badala ya fedha za Tanzania, kwa wanafunzi wa vyuo vikuu ambao ni wazawa.
“Je serikali inatoa tamko gani juu ya jambo hili?”alihoji.

Akijibu swali hilo, Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi Tekonolojia na Ufundi, Stella Manyanya, alisema  maagizo yaliyotolewa kwa wamiliki wa vyuo ni kuzingatia kanuni na taratibu zilizoweka.

Manyanya alisema  hakuna malalamiko kuhusiana na vyuo kutoza ada kwa watanzania kwa fedha za kigeni yaliyowasilishwa.

‘’Endapo kuna chuo chochote kinachotoza ada kwa watanzania kwa fedha za kigeni wapeleke taarifa rasmi Wizara ya Elimu ili hatua stahiki za sheria zichukuliwe dhidi ya wahusika,’’ alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
580,000SubscribersSubscribe

Latest Articles