29.3 C
Dar es Salaam
Thursday, June 1, 2023

Contact us: [email protected]

SABABU WANAWAKE KUATHIRIKA ZAIDI MAGONJWA YA FIGO, ZATAJWA


Na Veronica Romwald – Dar es Salaam


Hali ya ujauzito na kitendo cha kuvuja damu nyingi wakati wa kujifungua zimetajwa kuwa sababu zinazochangia wanawake kuugua magonjwa ya figo.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Faustine Ndugulile amesema hayo leo Machi 10, kwenye Maadhimisho ya Siku ya Figo Duniani.

“Magonjwa ya kisukari na shinikizo la damu nayo huchangia zaidi magonjwa haya, ikiwamo ulaji mbovu na kutokufanya mazoezi,” amesema.

Amesema ili kuwezesha wananchi kupata huduma ya kusafisha nchini serikali imeongeza vituo na kufikia jumla ya 17.

“Mgonjwa wa figo hawezi kuishi ikiwa hasafishwi damu (dialysis), zamani mtu alikuwa akiugua magonjwa haya anakufa lakini tukaweka juhudi na kuongeza huduma hii kwenye hospitali za serikali na za binafsi,” amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,225FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles