25.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

MAGUFULI: SITOI MITAJI NG’O KWENYE MABENKI

  • Ammwagia sifa, amwahidi nafasi Dk. Kimei

ALEX SAYI Na JUDITH NYANGE -GEITA /MWANZA


RAIS Dk. John Magufuli, amesema Serikali haitatoa fedha yoyote kwa benki zitakazoshindwa kujiendesha zenyewe, iwe ya wanaume, wanawake, vijana au ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kuwataka kuungana na benki nyingine ili waendelee kuwa na hisa.

Akizungumza jana wakati wa uzinduzi wa Tawi la Benki ya CRDB wilayani Chato mkoani Geita, Rais Magufuli, aliiagiza Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kuanza mchakato wa kuzifuatilia benki zote ambazo zinasuasua na zilizokuwa na mitaji ya Serikali ili kuzichukuwa.

Katika hilo alisema ni bora zikabaki benki chache zinazotoa huduma kwa wananchi masikini na kusisitiza zitakazoshindwa kujiendesha zenyewe basi nazo zitafungiwa.

Zaidi aliipongeza BoT kwa uamuzi wake wa kuzifungia benki zaidi ya tano na kutoa muda wa matazamio kwa nyingine tatu.

Akiizungumzia benki ya CRDB, Rais Magufuli, aliipongeza kwa kuwa miongoni mwa benki 50 zinazofanya vizuri kwa sasa kuwahudumia na kuwafikia wananchi katika kila eneo kwa kuwa na matawi zaidi ya 250 nchini huku ikitoa fursa ya ajira kwa Watanzania zaidi ya 4,000.

Kutokana na hilo, Rais Magufuli alieleza kuguswa na utendaji kazi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei, hivyo kumhakikishia ajira serikalini kwa asilimia 100 pindi atakapostaafu utumishi wake ndani ya benki hiyo.

Rais Magufuli alisema Dk. Kimei amefanya kazi nzuri ya kuijenga benki hiyo na hakuna mtu yeyote atakayepinga suala hilo.

“Umeijenga hii benki hakuna ambaye atapinga, wapo watu wamepewa matawi tu lakini yamewafia wamekuwa na maneno mengi kuliko vitendo, inawezekana usipendeke sana lakini ulikuwa mtendaji wa kuigwa, ulienda kufanya kazi kama kuna mapungufu na wewe ni binadamu lakini CRDB umeijenga na kuisimamia kwa dhati,” alisema.

Alisema amepata taarifa kuwa muda wa utendaji kazi wa Dk. Kimei ndani ya benki ya CRDB unakaribia kumalizika hivyo alimhakikishia kupata kazi serikalini kwa kuwa bado anaweza kuitumikia nchi na kumuahidi nafasi mbadala katika fani yake aliyobobea.

“Dk. Kimei naambiwa unamaliza muda wako, lakini muda ndani ya Serikali haujaisha, utakuwa unamaliza muda wako CRDB ila ndani ya Serikali upo, bahati nzuri unamaliza nikiwa rais wewe fanya kazi yako umalizie muda wako vizuri, I guarantee (ninakuhakikishia) asilimia 100 muda wako wa kuifanyia kazi Serikali hii haujaisha.

Inaendelea………………… Jipatie nakala yako ya gazeti la MTANZANIA

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles