28.4 C
Dar es Salaam
Sunday, April 28, 2024

Contact us: [email protected]

RPC awataka polisi kuwapigia saluti wabunge

Walter  Mguluchuma, Katavi



Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi, Damas Nyanda amewaagiza Askari Polisi wa mkoani hapa, kuhakikisha wanawapigia saluti wabunge wanapokuwa kwenye  majimbo yao kama maelekezo ya jeshi hilo yanavyoelekeza.

Kamanda Nyanda alitoa agizo hilo jana wakati   akizungumza na polisi wa ngazi mbalimbali wa mkoa huo wakati wa hafla ya kupokea msaada wa fenicha zikiwamo meza na viti vilivyotolewa na Mbunge wa  Jimbo la  Mpanda Mjini, Sebastian Kapufi (CCM), kwa  ajili ya Kituo cha Polisi cha Wilaya ya Mpanda.

“Ni vizuri mkatambua nafasi za waheshiwa wabunge kwani wapo baadhi ya askari hata wanapokuwa wanakutana na wabunge wamekuwa hawajali nafasi zao na wamekuwa hawawapigii saluti.

“GPO  namba 102 ya Jeshi la Polisi inaekekeza ni viongozi wapi wanaotakiwa kupigiwa saluti wakiwamo na wabunge lakini askari polisi wamekuwa baadhi yao hawapigii saluti wabunge wao, hivyo watambue kuwa wanafanya makosa, suala hili si hiari ni lazima,” amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles