23.1 C
Dar es Salaam
Sunday, September 8, 2024

Contact us: [email protected]

ROY HODGSON APEWA RASMI CRYSTAL PALACE

 

LONDON, ENGLAND

UONGOZI wa klabu ya Crystal Palace, umethibitisha kumpa mkataba wa miaka miwili aliyekuwa kocha wa timu ya Taifa ya England, , akichukua nafasi ya Frank De Boer aliyefukuzwa kazi mapema wiki hii.

De Boer amefukuzwa kazi baada ya timu hiyo kufungwa michezo yote minne ya Ligi Kuu nchini England tangu kufunguliwa kwa ligi, hivyo timu hiyo ikaamua kuvunja mkataba wake.

Kocha huyo amefukuzwa ikiwa ni siku 77 tangu uongozi wa timu hiyo umpe jukumu la kuwa kocha mkuu kwa mara ya kwanza baada ya msimu uliopita kufukuzwa katika kikosi cha matajiri wa nchini Italia, Inter Milan.

Baada ya Hodgson kusaini mkataba wenye thamani ya pauni milioni 2.5 kwa mwaka, alianza rasmi kibarua chake jana katika makao makuu yao ya Beckenham HQ.

Hata hivyo, Crystal Palace wamesema wanaweza kumwongezea kocha huyo mpya kitita cha pauni milioni moja endapo ataifanya klabu hiyo ibakie kwenye michuano ya Ligi Kuu msimu huu.

Hodgson ameamua kuongeza nguvu kwenye benchi lake la ufundi kwa kumchukua Ray Lewington, huku Sammy Lee ambaye alikuwa msaidizi wa Sam Allardyce na Frank de Boer, amewashiwa taa ya kijani kuwa anaweza kuondoka pamoja na wale wengine walikuwa chini ya kocha huyo.

“Ninayo furaha kurudi katika klabu hii ambayo nilianza maisha yangu ya soka nikiwa na umri mdogo, leo hii nimerudi tena ni jambo la kujivunia kwangu, nashukuru kwa kunipa nafasi hii,” alisema Hodgson.

Klabu ambazo amewahi kufundisha kocha huyo ni pamoja na Halmstad, Bristol City, Oddevold, Orebro, Malmo, Neuchatel Xamax, Switzerland, Inter Milan, Blackburn Rovers, Inter Milan, Grasshoppers, Copenhagen, Udinese, United Arab Emirates, Viking, Finland, Fulham, Liverpool, West Bromwich Albion na timu ya Taifa ya England.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles